Tuesday, February 11, 2014

IOC YAIRUDISHIA INDIA KITI CHAKE.

VIONGOZI wa Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa, IOC wameirejeshea India kiti chake baada ya kutimuliwa mwaka mmoja uliopita. India ilipigwa marufuku kutokana na shutuma kuwa serikali ilikuwa imeingilia kati uchaguzi wa kitaifa wa kamati ya olimpiki nchini humo. Kamati ya Olimpiki duniani iliagiza kufanyike mabadiliko ya katiba ya shirikisho la India mbali na kuruhusu uchaguzi huru na wa haki kufanyika. Hata hivyo kurejeshwa kwa India haitakuwa ahueni kwa wanariadha kutoka taifa hilo wanaoshiriki mashindano ya olimpiki ya msimu wa baridi huko Sochi Urusi chini ya bendera ya IOC badala ya taifa lao.

No comments:

Post a Comment