Tuesday, February 11, 2014

LIORIS ANAWEZA KUONDOKA SPURS - GIROUD.

MSHAMBULIAJI nyota wa Arsenal, Olivier Giroud amedai kuwa golikipa wa Tottenham Hotspurs Hugo Lloris anaweza kwenda Emirates katika majira ya kiangazi. Golikipa huyo wa kimataifa wa Ufaransa amewahi kuhusishwa na kwenda Arsenal wakati akiwa timu ya Olympique Lyon lakini badala yake akaenda kwa majirani zao Spurs. Hata hivyo Giroud mwenye umri wa miaka 27 amedokeza kuwa Lloris anaweza kuondoka kama Spurs wakishindwa kujihakikishia nafasi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa barani Ulaya. Giroud amesema wamekuwa marafiki na Lloris kwa kipindi kirefu na wamekuwa wakitoka pamoja na kuzungumza mengi ndio anajua kuwa anaweza kuondoka Spurs.

No comments:

Post a Comment