BEKI wa zamani wa Bayern Munich, Thomas Helmer anaamini kuwa Toni Kroos anakabiliwa na kibarua kigumu cha kuhakikisha anarejea katika kikosi cha kwanza cha kocha Pep Guardiola. Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 24 alipoteza nafasi yake katika kikosi cha kwanza baada ya kuonyesha kukasirishwa na kitendo cha kubadilishwa katika mchezo dhidi ya Stuttgart uliochezwa mwezi uliopita. Helmer amesema kama nyota huyo wa kimataifa wa Ujerumani hatajituma zaidi kuna uwezekano mkubwa akendelea kusugua benchi hata katika siku za mbele. Beki huyo aliendelea kudai kuwa Guardiola ana wachezaji wengi wa kuziba nafasi hiyo akiwemo Thiago Alcantara, Mario Gotze na Philipp Lahm hivyo asipojituma kuna uwezekano akakosa kabisa namba katika kikosi cha kwanza. Mkataba wa Kroos kukaa Bayern unamalizika Juni 2015 na pande zote mbili zimeshindwa kufikia makubaliano ya mkataba mpya kwasababu ya mshahara mkubwa anaohitaji mchezaji huyo.
No comments:
Post a Comment