Monday, February 17, 2014

BARCELONA SIO VIGOGO TENA ULAYA - LAHM.

MCHEZAJI nyota wa klabu ya Bayern Munich, Philipp Lahm amedai kuwa Barcelona sio timu kubwa tena barani Ulaya kuelekea katika mechi za hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa inayaotarajiwa kuanza kutimua vumbi kesho. Bayern waliidhalilisha Barcelona msimu uliopita kwa kuwaondoa kwa jumla ya mabao 7-0 katika mechi mbili za nusu fainali walizokutana na kutinga fainali ambapo waliwagaragaza Wajerumani wenzao Borussia Dortmund kwa mabao 2-1 katika fainali iliyochezwa Wembley. Lahm ambaye timu yake ya Bayern imepangwa na Arsenal katika hatua hiyo kwa msimu wa pili mfululizo, hadhani kama Barcelona wana nguvu kama walivyofanya wakati wakinolewa na Pep Guardiola. Nyota huyo amesema katika miaka ya karibuni Barcelona ndio walikuwa wkaipewa nafasi ya kunyakuwa taji hilo mara nyingi lakini sasa hivi kibao kimegeuka kwasababu Bayern ndio watetezi. Bayern itakuwa wageni wa Arsenal katika Uwanja wa Emirates Jumanne huku ikiwakosa nyota wake wawili ambao ni majeruhi Xherdan Shaqiri na Franck Ribery.

No comments:

Post a Comment