MENEJA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amethibitisha kuwa hatua za kinidhamu zitachukuliwa dhidi ya Olivier Giroud baada ya kuomba radhi kwa kumuingiza mwanamke katika chumba cha hoteli ilipofikia timu hiyo. Mara kwa mara Giroud amekuwa akikataa kumchukua Celia Kay katika Hotel ya Four Seasons iliyopo Canary Wharf usiku mmoja kabla ya mchezo wao dhidi ya Crystal Palace ambao walishinda mabao 2-0 Februari 2 mwaka huu. Mapema nyota huyo aliandika katika ukurasa wake wa mtandao wake wa kijamii wa twitter akimuomba radhi mke wake Jennifer na bosi wake Wenger baada ya picha ya mrembo huyo kutokea katika gazeti. Akihojiwa Wenger amesema suala hilo ni la ndani hivyo hataki kuliweka hadharani kwasababu anaheshimu mambo yake binafsi. Picha iliyopigwa na mrembo huyo katika chumba alichofikia Giroud akiwa na nguo ya ndani pekee ilichapishwa katika gazeti la The Sun Jumapili iliyopita. Mrembo huyo mwanamitindo wa majarida ya kimataifa kama Maxim na FHM alipigwa picha akiingia hotelini hapo akiingia na akitoka katika mida mibovu ya usiku wa manane huku mwenyewe akimshangaa Giroud kukana kujirusha naye usiku huo.
No comments:
Post a Comment