Tuesday, February 4, 2014

CHELSEA HAINA MPANGO NA UBINGWA WA LIGI KUU - MOURINHO.

MENEJA wa klabu ya Chelsea, Jose Mourinho amepuuzia madai kwamba kikosi chake ndio kinachopewa nafasi ya kunyakuwa taji la Ligi Kuu nchini Uingereza baada ya kuigaragaza Manchester City kwa bao 1-0 katika Uwanja wa Etihad jana usiku. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo, Mourinho amesema kwasasa anatengeneza kikosi kwa ajili ya msimu ujao hivyo taji la ligi haliko katika mipango yake kwasasa ingawa wakifanikiwa kulichukua itakuwa ni hatua nzuri. Mourinho pia alikisifu kikosi chake kwa kucheza mchezo mzuri na pia kutengeneza nafasi nyingi ambazo zingeweza kumaliza mchezo huo mapema kulinganisha na wapinzania wao. Hii ni mara ya kwanza kwa City kushindwa kufunga bao wakiwa nyumbani toka walipotoka sare ya 0-0 na Birmingham City Novemba 2010.

No comments:

Post a Comment