MFANYAKAZI wa Ujenzi amefariki dunia kaskazini mwa Brazil katika ajali ya mojawapo ya viwanja vinavyojengwa kwa ajili ya michuano ya Kombe la Dunia inayotarajiwa kuanza Juni mwaka huu. Mfanyakazi huyo ambaye ni raia wa Ureno aliumia kichwani wakati akifungua crane nje ya Uwanja wa Arena da Amazonia uliopo katika mji wa Manaus. Huyo anakuwa ni mtu wa tatu kufariki katika ajali wakati wa ujenzi wa viwanja vitakavyotumika kwa ajili ya michuano hiyo. Katibu wa kamati ya maandalizi ya mji huo, Miguel Capobiango amesema crane hilo lilikuwa likifunguliwa baada ya sehemu ya ujenzi wa uwanja huo kukamilika. Uwanja huo unatarajiwa kuchezwa mchezo wa ufunguzi kati ya Uingereza na Italia.
No comments:
Post a Comment