Friday, February 7, 2014

MWAMUZI ALIYEMPA RONALDO KADI NYEKUNDU AFUNGIWA.

MWAMUZI ambaye alimtoa Cristiano Ronaldo katika mchezo ambao Real Madrid ilitoa sare dhidi ya Athletico Bilbao mwishoni mwa wiki iliyopita, amefungiwa. Kamati ya Ufundi ya Wamuzi wa Ligi Kuu nchini Hispania, CTA imemfungia Miguel Angel Ayza Gamez kwa mwezi mmoja huku akizuiwa kuchezesha mechi za Madrid msimu huu. Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na vyombo vya habari nchini Hispania zimedai kuwa kuna uwezekano mkubwa mwamuzi huyo akaenguliwa katika orodha ya waamuzi wa La Liga kutokana na maamuzi yake mabovu. Ronaldo alitolewa nje kwa kadi nyekundu katika dakika ya 75 ya mchezo huo ikiwa ni mara ya saba toka aanze kucheza soka baada ya kumpiga konzi nahodha wa Bilbao Carlos Gurpegi ambaye alianguka chini kwa maumivu. Kwa tukio hilo pamoja na kusukumana na kiungo wa Bilbao Ander Iturraspe imepelekea Ronaldo kufungiwa mechi tatu za La Liga ambapo atakosa mechi kati ya timu yake dhidi ya Villareal, Getafe na Elche. Hata hivyo habari za kufungiwa kwa mwamuzi huyo kutawapa nguvu Madrid kukata rufani kwa adhabu aliyopewa Ronaldo.

No comments:

Post a Comment