MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Brazil, Neymar amemtetea baba yake kuhusiana na sakata la uhamisho wake kutoka Santos kwenda Barcelona. Kampuni ya N&N ambayo inamilikiwa na wazazi wa nyota huyo mwenye umri wa miaka 21 ilipokea kiasi cha euro milioni 10 mwaka 2011 ili kuhakikisha kuwa Neymar haondoki Santos kwenda katika klabu yoyote ila Barcelona. Malipo hayo ni sehemu ya euro milioni 40 ambazo Barcelona ililipa kwa ujumla ili kuhakikisha wanapewa nafasi ya kwanza kama ukifanyika uhamisho wowote. Neymar alituma ujumbe katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram kwamba hawezi kunyamaza kimya na kuacha watu waseme vibaya kuhusu familia yake wakati hawajafanya lolote baya. Nyota huyo amesema alikaa kimya kipindi kirefu kwasababu baba yake alimwambia afanye hivyo nay eye anashughulikia tatizo hilo lakini ameshindwa baada ya kuona tuhuma dhidi ya familia yake zinazidi. Kwasasa yuko benchi akikiuguza kifundo cha mguu.
No comments:
Post a Comment