Friday, February 7, 2014

OLIMPIKI YA MAJIRA YA BARIDI YAANZA KUANZA RASMI SOCHI.

SHEREHE za ufunguzi wa michuano ya olimpiki ya majira ya baridi zinafanyika leo jijini Sochi, Urusi huku kukiwa na tahadhari kubwa ya mambo ya kiusalama. Mji wa Sochi uliopo katika pwani ya Bahari Nyeusi, unatarajiwa kukaribisha zaidi wa wanariadha 2,900 ambao watakuwa wakigombea medali 98 katika michezo mbalimbali itakayokuwepo katika michuano hiyo ya siku 16. Wakati watu wakiwa na hamasa katika ufunguzi wa michuano hiyo kumekuwa tahadhari kubwa ya mambo ya kiusalama huku serikali ya Marekani ikionya mashirika ya ndege yanayosafiri kwenda Urusi kuwa waangalifu. Marekani wanahisi huenda magaidi wakatumia dawa za kusugua meno kupitisha vilipuzi kimagendo kwa ajili ya kutimiza haja zao za kigaidi. Ofisa mmoja wa Idara ya Usalama ya Marekani amesema vilipuzi hivyo vinaweza kutumiwa kutengeeza bomu ndani ya ndege au baada ya kuwasili katika michuano hiyo. Vikosi vya usalama vya Serikali ya Urussi viko katika hali ya tahadhari baada ya makundi ya wanamgambo na magaidi kutishia kufanya mashambulizi katika mashindano ya Olimpiki ya msimu wa baridi ya Sochi.

No comments:

Post a Comment