Friday, February 7, 2014

MESSI ATUHUMIWA KUPOTEZA MAPENZI NA SOKA.

KOCHA msaidizi wa zamani wa Barcelona, Angel Cappa amemtuhumu Lionel Messi kupoteza mapenzi na soka. Muargentina huyo mwenye umri wa miaka 67 ambaye alifanya kazi chini ya Cesar Luis katika miaka ya themanini amedai kuwa kiwango cha Messi alichoonyesha katika mchezo wa Jumamosi ambao walipata kipigo cha mabao 3-2 kutoka kwa Valencia ni ushahidi tosha wa anachokisema. Cappa anadhani kuwa kuwa Messi alikuwa na morari zaidi katika mchezo wa Jumatano usiku wa Kombe la Mfalme dhidi ya Real Sociedad lakini bado anaona nyota huyo bado anahitaji kurejesha mapenzi yake katika soka. Kocha huyo amesema ili ucheze soka unatakiwa uwe na mapenzi ya kweli kama ilivyokuwa kwa kina Diego Maradona na wachezaji wengine mahiri waliopo na wa zamani na Messi anahitaji kurejesha mapenzi yake ili aweze kurudi katika kiwango chake.

No comments:

Post a Comment