MENEJA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amebainisha kuwa Mesut Ozil anatarajia kurejea katika kikosi cha timu hiyo wakati watakapoifuata Stoke City katika mchezo wa Ligi Kuu utakaochezwa Jumamosi. Nyota huyo wa kimataifa wa Ujerumani aliachwa katika kikosi kilichoshinda mabao 4-1 dhidi ya Sunderland kufuatia kiwango kibovu alichocheza katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Bayern Munich ambao ulishuhudia akikosa penati dakika za mwanzoni. Wenger alipuuza taarifa kuwa alimuacha Ozil kutokana na kushuka kiwango na kusisitiza kuwa alimuacha kiungo huyo apumzike kutokana na mchezo mgumu dhidi ya Bayern na sasa mchezaji huyo sambamba na Thomas Vermaelen watarejea kwenye mchezo dhidi ya Stoke. Kocha huyo amesema mchezo dhidi ya Bayern ulikuwa mgumu hivyo ni muhimu kumpa mchezaji mapumziko haswa anapokuwa katika shinikizo.
No comments:
Post a Comment