KIUNGO mahiri wa klabu ya Barcelona, Xavi Hernandez ameonyesha kuchanganyikiwa kwa kupunguziwa muda wa kucheza chini ya kocha mpya Gerardo Martino msimu huu lakini amesisitiza kuwa hatasababisha matatizo yoyote kutokana na mabadiliko hayo. Xavi mwenye umri wa miaka 34 alicheza dakika zote tisini katika mechi tisa kati ya 25 za ligi alizocheza msimu huu huku akishindwa kuchomoza katika kikosi cha kwanza, amekiri kuwa sio rahisi kupambana na hali hiyo mpya. Akihojiwa nyota huyo amesema ni jambo linalomchanganya wakati anapokosa muda wa kucheza lakini siku zote anaheshimu maamuzi ya kocha ambaye ndo mwenye uamuzi wa mwisho. Xavi aliendelea kusema kuwa katika kikosi cha Barcelona wachezaji wote wanajua hakuna aliyekuwa juu ya kocha.
No comments:
Post a Comment