RAIS wa klabu ya Lazio, Claudio Lotito amedai kupokea zaidi ya vitisho 50 vya kifo toka klabu hiyo imuuze kiungo wake Hernanes kwenda Inter Milan siku ya mwisho kabla dirisha dogo la usajili halijafungwa. Lotito aliwaambia waandishi wa habari kuwa amepokea simu kati ya 50 mpaka 80 kutoka kwa mashabiki ambao walimpataka aondoke Lazio na kutoa vitisho vya kumuua. Rais huyo amesema kwasasa anaishi chini ya ulinzi mkali na kuwa mashabiki ni sehemu ya klabu lakini sasa anadhani kuwa wmaevuka mipaka. Mbali na vitisho hivyo vya hivi karibuni lakini pia Lotito amesema amewahi kupokea vitisho Septemba mwaka jana baada ya klabu hiyo kushindwa kumsajili beki wa Uturuki Burak Yilmaz kutoka klabu ya Galatasaray. Lotito amesema mashabiki wanapaswa waelewe kuwa hakuna kitu wangeweza kufanya ili kuzuia Hernanes ambaye ni raia wa Brazil kuondoka kwenda Milan.
No comments:
Post a Comment