RIBERY KUUKOSA MCHEZO DHIDI YA ARSENAL.
KIUNGO mahiri wa klabu ya Bayern Munich Franck Ribery anatarajia kuukosa mchezo wa mkondo wa Ligi ya Mabingwa barani Ulaya hatua ya timu 16 bora dhidi ya Arsenal kufuatia kufanyiwa upasuaji wa makalio. Nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 30 alifanyiwa upasuaji Februari 6 mwaka huu ili kuondoa uvimbe uliokuwa umeota katika makalio yake. Taarifa iliyotolewa na klabu hiyo imedai kuwa Ribery atakuwa fiti katika mchezo wa mkondo wa pili huku akitarajiwa kuanza mazoezi mepesi wiki ijayo. Bayern itakabiliwa na mchezo dhidi ya Arsenal Februari 19 kabla ya kurudiana tena nchini Ujerumani Machi 11 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment