MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Borussia Dortmund, Robert Lewandowski Jumatatu ya wiki hii ilianza vibaya kwake baada ya kuamka na kukuta gari lake la kifahari aina ya Porsche likiwa juu ya mawe baada ya kuibiwa baadhi ya vitu vyake. Gari hilo linalokadiriwa kuwa na thamani ya euro 96,000 lililokuwa limepaki nje ya nyumba yake lilivamiwa na watu wasiojulikana na kuvuliwa matairi yote manne huku likiachwa juu yam awe. Nyota huyo mwenye miaka 25 amekuwa sehemu muhimu ya kikosi cha Jurgen Klopp katika misimu ya hivi karibuni huku akirejesha makali yake ya kufumania nyavu kwa kufunga bao lake la 18 msimu huu katika ushindi wa mabao 5-1 iliyopata Dortmund dhidi ya Werder Bremen. Hata Hivyo, Lewandowski ambaye ni raia wa Poland tayari ameshasajiliwa na Bayerm Munich ambao anatarajiwa kujiunga nao katika majira ya kiangazi. Bado haijathibitika kama uhalifu huo umefanywa mashabiki wa Dortmund, ambao bado wana hasira na kuondoka kwa Mario Gotze kwenda Bayern katika majira ya kiangazi mwaka jana. Hilo tukio la kwanza kumhusisha Lewandowski toka alipobainisha kuwa yeye ni mali ya Bayern.
No comments:
Post a Comment