Wednesday, February 5, 2014

RONALDO AFUNGIWA MECHI TATU.

CHAMA cha Soka nchini Hispania, RFEF kimfungia mechi tatu nyota wa klabu ya Real Madrid Cristiano Ronaldo kufuatia kadi nyekundu aliyoonyeshwa katika mchezo dhidi ya Atletico Bilbao. Nyota huyo wa kimataifa wa Ureno ambaye anasheherekea siku yake ya kuzaliwa leo alitolewa nje katika dakika ya 76 baada ya kuzozana na wachezaji wa Bilbao Ander Iturraspe na Carlos Gurpegui. Katika taarifa yake RFEF imesema imempa adhabu ya kumfungia mechi moja kwa tukio lake na Iturraspe lakini inamuongeza mechi zingine kwa tabia aliyoonyesha baada ya kupewa kadi nyekundu. Nyota huyo anatarajiwa kukosa mechi za La Liga dhidi ya Villarreal utakaochezwa Februari 9, Elche utakaochezwa Februari 23 pamoja na mchezo dhidi ya Getafe utakaochezwa Februari 16.

No comments:

Post a Comment