KIUNGO wa klabu ya Real Madrid, Luka Modric anaamini kuwa Cristiano Ronaldo ameadhibiwa isivyo hali kwa kadi nyekundu aliyopewa katika mchezo dhidi ya Athletico Bilbao. Nyota huyo wa kimataifa wa Ureno alifungiwa mechi tatu kufuatia kadi nyekundu hiyo aliyopewa na kumfanya kukosa mechi tatu dhidi ya Villareal, Getafe na Elche. Modric amesema kufungiwa kwa Ronaldo sio halali kwasababu hakuna kitu chohcote kibaya alichofanya katika tukio hilo lililopelekea kutolewa nje. Nyota huyo wa zamani wa Tottenham Hotspurs amesema hawawezi kufanya chochote ila wanatakiwa kufanya kazi zaidi kipindi hiki wakati Ronaldo hachezi kwasababu ni mchezo muhimu katika kikosi chao. Madrid wanatarajiwa kuikwaa Villareal Jumapili katika Uwanja wa Santiago Bernabeu.
No comments:
Post a Comment