MENEJA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amepanga kuvunja benki na kusajili wachezaji watatu nyota katika kipindi cha usajili majira ya kiangazi. Kumekuwa na tetesi kuwa Wenger amepanga kusajili beki mpya wa kati, kiungo wa kati na mshambuliaji mara tu dirisha dogo la usajili litakapofunguliwa. Tayari maskauti wa klabu hiyo wameshasambazwa ili kutafuta wachezaji walengwa ambao wataziba nafasi ambazo Wenger anataka kuongeza nguvu katika kikosi chake. Pamoja na kumsajili Mesut Ozil katika majira ya kiangazi mwaka jana kwa paundi milioni 42, timu hiyo bado ina fungu kubwa la usajili baada ya kusaini mikataba kadhaa ya matangazo. Wenger tayari amewaweka nyota kadhaa katika rada zake wakiwemo Jackson Martinez, Edin Dzeko, Mario Mandzukic na Diego Costa huku beki wa Borussia Dortmund Likasz Piszczek naye akitazamwa kwa karibu.
No comments:
Post a Comment