NAHODHA wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza, David Beckham amesema anaishi katika ndoto zake baada ya kubainisha mipango yake ya kumiliki timu katika Ligi Kuu nchini Marekani, MLS. Beckham mwenye umri wa miaka 38 ambaye alistaafu kucheza soka Mei mwaka jana anataka kutafuta wachezaji nyota ili kumsaidia kutengeneza klabu yake mpya itakayopendwa na mamilioni ya mashabiki. Nyota huyo amesema uwanja mpya wenye hadhi ya kimataifa unatarajiwa kujengwa kwa ajili ya klabu hiyo ambayo itakuwa ya 22 katika MLS. Beckham ambaye amewahi kucheza katika vilabu vya Manchester United, Real Madrid, AC Milan, Los Angeles Galaxy na Paris Saint-Germain amesema anataka kuifanya timu hiyo kuwa yak wake. Mpaka sasa hakuna tarehe rasmi iliyotajwa ya timu hiyo kujiunga na MLS.
No comments:
Post a Comment