MAHAKAMA ya Sifa nchini Misri imeagiza kurudiwa kwa hukumu ya kifo waliyopewa watu 21 kutokana na kuhusishwa na vurugu katika soka zilizotokea huko Port Said mwaka 2012. Watu wapatao 74 wengi wao wakiwa mashabiki wa klabu ya Al Ahly yenye maskani yake jijini Cairo, waliuawa wakati kulizuka vurugu katika mechi dhidi ya klabu ya Al Masry. Baadhi ya wadau wamekuwa wkailalamikia adhabu iliyotolewa na kudai kuwa hukumu ilikuwa imekaa kisiasa zaidi. Alhamisi wiki hii Mahakama ya Sifa ilikubali rufani ya mashabiki hao wlaiokutwa na hatia ya kuhusika na vifo vya watu waliopoteza maisha katika tukio hilo lililotokea Februari mosi mwaka 2012. Watu wengi walikufa kwa kukanyagana wakati mashabiki wakitaribu kukimbia huku na kule ili kunusuru maisha yao katika Uwanja wa Port Said baada ya mashabikiwa Al Masry kuvamia uwanjani kushangiliwa ushindi wa timu yao.
No comments:
Post a Comment