MKURUGENZI wa klabu ya Barcelona, Susana Monje amekiri kuwa sakata la uhamisho wa Neymar kwenda Camp Nou ndio sababu kubwa ya kujiuzulu Sandro Rosell nafasi ya urais wa klabu hiyo. Rosell mwenye umri wa miaka 49 aliachia nafasi hiyo mwishoni mwa Januari mwaka huu akidai vitisho vya vurugu dhidi ya familia yake kutokana na sakata hilo la uhamisho. Monje ambaye ni mkurugenzi wa mambo ya uchumi wa klabu hiyo amesema sakata la uhamisho huo ndio limepelekea Rosell kujiuzulu na amepania kuhakikisha hakutokea usajili wenye katika siku za usoni. Monje amekiri usajili wa Neymar ulikuwa na utata na ana mategemeo hawataingia katika tatizo kama hilo tena.
No comments:
Post a Comment