BEKI wa kimataifa wa Vietnam Tran Dinh Dong amepewa adhabu iliyovunja rekodi ya kufungiwa mechi 28 na Shirikisho la Soka la nchi hiyo kwa kumvunja mguu mchezaji mwenzake kwenye mchezo wa ligi. Dong anayecheza katika timu ya Song Lam Nghe An pia alipigwa faini ya dola 950 kwa kumkwatua na kumvunja Hung Vuong An Giang ambaye anacheza timu ya Nguyen Anh Hung. Dong ambaye hategemewi kurejea uwanjani mwaka huu amesema atakata rufani kupinga adhabu ambayo pia imehusisha kumlipia gharama za matibabu mchezaji aliyemvunja. Naye kocha wa timu ya Dong, Nguyen Huu Thang amesema shirikisho hilo halikutenda haki kwani inaonekana wametoa adhabu hiyo kwa msukumo kutoka kwa watu.
No comments:
Post a Comment