MMILIKI wa klabu ya Birmingham City ya Uingereza, Carson Yeung amekutwa na hatia na mahakama ya Hong Kong kwa makosa matano ya kuchakachua fedha ambazo zimemfanya kuwa tajiri. Yeung ambaye amekana makosa hayo ya kuchakachua kiasi cha dola milioni 93 kati ya Januari mwaka 2001 na Desemba 2007, anatarajiwa kuhumiwa Ijumaa na anaweza akahukumiwa miaka saba jela. Tajiri huyo ambaye alikuwa mtaalam wa kutengenza nywele watu matajiri na maarufu huko Hong Kong aliiambia mahakama kuwa ametengeneza utajiri wake kupitia shughuli za kutengeneza nywele, kununua hisa, kununua nyumba, kucheza kamari pamoja na uwekezaji mwingine. Jaji aliyekuwa akisikiliza kesi iliyochukua muda wa siku 50 amesema amemkuta na hatia Yeung kwa kuidanganya mahakama jinsi alivyopata utajiri wake kwa kupitia utengenezaji nywele na kamari.
No comments:
Post a Comment