MSHAMBULIAJI wa klabu ya Olympiakos Michael Olaitan anaendelea vizuri katika hospitali aliyolazwa nchini Ugiriki baada ya kuanguka katika kipindi cha kwanza katika mchezo dhidi ya mahasimu wao wa jiji la Athens Panathiakos. Nyota huyo wa kimataifa wa Nigeria mwenye umri wa miaka 21 alikuwa akikokota mpira wakati alipoanguka na kuzimia. Mapema katika mchezo huo meneja wa Panathiakos Yannis Anastasiou naye alianguka baada ya kupigwa kitu kilichorushwa kutoka kwa mashabiki. Olaitan ambaye aliisadia Olympiakos kuichapa Manchester United mabao 2-0 katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa barani Ulaya uliochezwa Februari 25 mwaka huu, alizinduka kabla hajapelekwa hospitalini kwa matibabu zaidi.
No comments:
Post a Comment