MENEJA wa klabu ya Chelsea, Jose Mourinho ametamba kuwa kikosi chake kimerejea katika nafasi yake barani Ulaya baada ya kutinga hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa. Chelsea imeigaragaza Galatasaray kwa mabao 2-0 katikia Uwanja wa Stamford Bridge hivyo kutinga hatua hiyo kwa jumla ya mabao 3-1. Mourinho amesema kwa majigambo kuwa Chelsea ni mojawapo ya vilabu bora duniani kwasababu imetinga hatua hiyo muhimu katika michuano hiyo. Chelsea inaweza kuwa timu pekee itakayopeperusha bendera ya Uingereza katika michuano hiyo baada ya Manchester City na Arsenal kutolewa huku Manchester United wakiwa nyuma kwa mabao 2-0 kuelekea mchezo wao dhidi ya Olympiakos. Mourinho amesema kutoka kushinda taji la Europa League mpaka kutinga robo fainali ya Ligi ya Mabingwa ni hatua kubwa kwa klabu na wachezaji wa timu hiyo.
No comments:
Post a Comment