MKURUGENZI wa michezo wa klabu ya Bayern Munich, Matthias Sammer anafikiri vilabu vingine vya Bundesliga vinaona wivu kwa mafanikio waliyopata katika miaka ya karibuni. Bayern imekuwa klabu inayoogopewa barani Ulaya katika miezi 18 iliyopita lakini wamekuwa wakishambuliwa nchini Ujerumani kwa sera yao ya usajili ambayo inakandamiza vilabu vingine visivyouwa na hela. Sammer amesema katika kipindi cha miezi 18 iliyopita Bayern imeshinda mataji sita, badala ya kuzungumzia mafanikio klabu zingine zimekuwa zikiona wivu na kujaribu kuwafanya kuonekana wabaya. Nguli huyo wa soka wa zamani wa Ujerumani amesema siri kubwa ya mafanikio ya Bayern ni kufanya mazoezi kwa bidii na kuhakikisha wachezaji wao wanachezaji katika kiwango bora kipindi chote.
No comments:
Post a Comment