MCHEZAJI tenisi namba moja nchini Uingereza, Andy Murray ameamua kumtimua kocha wake Ivan Lendl baada ya kukaa nae kwa kipindi cha miaka miwili. Akiwa chini Lendl, Murray mwenye umri wa miaka 26 alifanikiwa kushinda taji moja la Grand Slam na medali ya dhahabu katika mashindano ya olimpiki mwaka 2012 na baadae kushinda taji la Wimbledon mwaka jana. Katika taarifa yake Murray amesema anashukuru kwa kazi kubwa ambayo Lendl amekuwa akiifanya, amejifunza mengi kutoka kwake na anategemea yatamsaidia katika siku za baadae. Naye Lendl alishukuru kwa kufanya kazi na nyota huyo na kumsifu kuwa mmoja wa wachezaji bora kabisa wa tenisi duniani. Murray ambaye kwasasa yuko jijini Miami, Marekani akijiandaa kutetea taji lake la Masters amesema amepanga kuchukua muda kabla ya kuamua kutafuta kocha mwingine.
No comments:
Post a Comment