MCHEZAJI wa zamani wa kimataifa wa Ujerumani Magharibi na klabu ya Real Madrid, Uli Stielike anaamini kuwa kikosi cha Carlo Ancelotti kitachuana na Barcelona katika mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya. Bayern ndio mabingwa watetezi wa michuano hiyo na tayari wameshakata tiketi ya kucheza hatua ya robo fainali baada ya kuiondosha Arsenal kwa jumla ya mabao 3-1. Madrid nao wako katika nafasi nzuri ya kusonga mbele baada ya kuigaragaza Schalke kwa mabao 6-1 katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa michuano hiyo na Stielike mwenye umri wa miaka 59 aliyecheza Madrid kwa miaka nane anaamini timu hizo mbili ndio bora barani Ulaya hivi sasa. Nguli huyo amesema kwa vikosi vya timu hizo mbili hakuna shaka kwamba ndio vilabu bora Ulaya kwasasa na itakuwa fainali nzuri kama zikicheza timu hizo.

No comments:
Post a Comment