MENEJA wa klabu ya Chelsea, Jose Mourinho anaamini nguli wa zamani wa timu hiyo Didier Drogba bado ni mmoja ya washambuliaji bora kabisa duniani. Mshambuliaji huyo anayecheza klabu ya Galatasaray ambaye aliondoka Stamford Bridge Juni mwaka 2012 anarejea jijini London kwa ajili ya mchezo wa mkondo wa pili wa Ligi ya Mabingwa Ulaya utakaochezwa leo usiku. Mourinho amesema Drogba ambaye kwasasa ana umri wa miaka 36 bado na mchezaji yuleyule kama alivyokuwa wakati ana umri wa miaka 26 kitu ambacho unaweza kukipata kwa wachezaji wachache. Drogba mwenyewe amesema anaweza asishangilie kama atafunga bao katika mchezo huo dhidi ya timu yake hiyo ya zamani. Nyota huyo wa kimataifa wa Ivory Coast ametupia mabao 157 katika mechi 342 alizocheza katika kipindi cha miaka nane aliyokaa Chelsea.

No comments:
Post a Comment