Friday, March 14, 2014

HATIMAYE KALLSTROM ATARAJIWA KULIOKOA JAHAZI LA ARSENAL DHIDI YA TOTTENHAM.

KIUNGO Kim Kallstrom anaweza kucheza mechi yake ya kwanza akiwa na Arsenal katika mchezo wa Jumapili ambao utawakunanisha na mahasimu wao Tottenham Hotspurs. Nyota huyo wa kimataifa wa Sweden mwenye umri wa miaka 31 hajacheza mechi yoyote toka asajiliwe na Arsenal katika kipindi cha dirisha dogo la usajili Januari mwaka huu. Kallstrom alisajiliwa na Arsenal akiwa majeruhi lakini akizungumzia safari yao ya White Hart Lane meneja Arsene Wenger amebainisha kuwa kiungo huyo ameanza mazoezi. Wenger amesema pamoja na kuanza mazoezi lakini bado ataamua kama ataweza kumtumia katika mchezo wa Jumapili au la. Wenger pia amesema Mesut Ozil ambaye alipata majeraha ya msuli katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Bayern Munich atakaa nje yaw a uwanja kwa kipindi kisichozidi wiki sita.

No comments:

Post a Comment