Friday, March 14, 2014

WENGER APUUZA TETESI ZA KWENDA BARCELONA.

MENEJA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amejiweka mbali na taarifa kutoka nchini Hispania kuwa anawindwa na Barcelona kwenda kuziba pengo la Tata Martino. Tetesi hizo na Wenger kwenda Catalunya zimeibuka kutokana na klabu hiyo kuwa katika kipindi kigumu baada ya kuporomoka mpaka nafasi ya tatu katika msimamo wa La Liga kutokana na vipigo viwili katika mechi tatu walizocheza. Hata hivyo Wenger alikanusha habari hizo na kudai kuwa majukumu yake yapo Arsenal na sio mahali pengine kokote. Wenger tayari amekubali mkataba mpya wa kuendelea kubakia Emirates toka Octoba mwaka jana lakini bado hajasaini mkataba huo rasmi.

No comments:

Post a Comment