RAIS wa klabu ya Bayern Munich, Uli Hoeness amejiuzulu wadhifa wake huo na kubainisha kuwa hana mpango wa kutaka rufani ya kufungwa jela miaka mitatu na nusu kwa kosa la ukwepaji kodi. Baada ya kushitakiwa kukwepa kulipa kodi ya euro milioni 3.5, Hoeness alikiri baadae kukwepesha kiasi cha paundi milioni 27.2 kutoka serikali ya Ujerumani na alihukumiwa jana. Ingawa wanasheria wake wamedai kumkatia rufani mteja wao, Hoeness mwenyewe amesisitiza atakubali hukumu aliyopewa na mahakama. Katika taarifa yake Hoeness amesema baada ya kuzungumza na familia yake ameamua kukubali maamuzi ya mahakama na tayari ameshawasiliana na mawakili wake kutokukata rufani.

No comments:
Post a Comment