Thursday, March 13, 2014

RAMSEY KUIKOSA SPURS.

KIUNGO wa klabu ya Arsenal, Aaron Ramsey hategemewi kuwepo katika kikosi cha timu hiyo kitakachopambana na mahasimu wao wa jiji la London Tottenham Hotspurs mwishoni mwa wiki hii. Arsenal wamekuwa na mategemeo kwamba kiungo huyo anaweza kurejea katika mchezo huo wa Jumapili ambao watakuwa wageni wa Spurs katika Uwanja wa White Hart Lane. Wiki iliyopita kocha wa Arsenal, Arsene Wenger alisema anategemea nyota huyo kuwa amepona kabisa baada ya wiki moja lakini hali imekuwa tofauti kwani amekuwa akipona taratibu. Ili kuhakikisha hawamharakishi kurejea uwanjani Wenger ameamua kumtegemea kiungo huyo katika mchezo wa ligi dhidi ya Chelsea utakaochezwa siku sita baadae.


No comments:

Post a Comment