Wednesday, March 5, 2014

JOHNSON AMPAKA MOURINHO.

BEKI wa klabu ya Liverpool, Glen Johnson amesema Brendan Rodgers ndio meneja bora kuliko Jose Morinho na kudai kuwa amepotza heshima aliyokuwa nayo kwa kocha huyo wa Chelsea wakati akiwa Stamford Bridge. Nyota huyo wa kimataifa wa Uingereza ambaye amecheza chini ya Mourinho kati ya mwaka 2004 na 2006 amesema haamini kama kocha huyo anaweza kutekeleza ahadi zake. Johnson ambaye alisaini Chelsea akiwa na umri wa miaka 18 amesema ilikuwa kazi ngumu kucheza chini Mourinho kwasababu kuna wakati alikuwa akimwambia kuwa anastahili kucheza kutokana na ubora wake. Beki anasema Mourinho alishindwa kutimiza ahadi alizompa kwmaba akicheza kwa bidii na kiwango juu basi atajihakikishia namba lakini haikuwa hivyo katika mechi kubwa na muhimu jambo ambalo lilirudisha nyuma kasi yake. Amesema kwa upande wa Rodgers mambo ni tofauti kwani kama ukionyesha kiwango kizuri unaweza kucheza hata katika mechi ubwa kama unastahili.

No comments:

Post a Comment