Wednesday, March 5, 2014

RAUL ANAWEZA KUWA KOCHA WA MADRID - VALDANO.

MKURUGENZI wa zamani wa klabu ya Real Madrid Jorge Valdano anaamini kuwa Raul anaweza kurejea Santiago Bernabeu kama kocha mkuu katika siku zijazo na kujitengenezea jina kama ilivyo kwa Pep Guardiola. Raul aliondoka Madrid na kuhamia Schalke mwaka 2010 kabla ya kuondoka katika timu hiyo ya Ujerumani na kwenda Al Sadd miaka miwili baadae lakini Valdano hana shaka kwamba mshambuliaji huyo mkongwe mwenye umri wa miaka 36 anaweza kurejea kuingoza klabu hiyo kwa mafanikio kama iliyokuwa alipokuwa mchezaji. Valdano amesema hana shaka kwamba hivi Raul anajipima kama anaweza kurejea Madrid akiwa kocha kwani anaweza kuongeza kitu muhimu kwa timu hiyo. Guardiola ambaye amewahi kucheza Barcelona alirejea tena katika timu hiyo akiwa kocha kati ya mwaka 2008 na 2012 akishinda mataji 14 kabla ya kuamua kupumzika kwa muda wa mwaka mmoja na kurejea kuinoa Bayern Munich.

No comments:

Post a Comment