LIGI Kuu nchini Italia inayojulikana kama Serie A imekuwa taratibu ikiporomoka kutoka katika nafasi yake ya mojawapo ya ligi bora barani Ulaya lakini inaweza inaweza kupata ahueni. Katika miaka michache iliyopita matukio ya upangaji matokeo, upungufu wa mashabiki na kuanguka kwa vilabu vikubwa kama AC Milan vimeifanya ligi hiyo kupoteza umaarufu wake.
Lakini soka la Italia linaweza kuanza kunyanyuka tena na mashabiki kuongezeka kama ilivyokuwa zamani kutokana na kuibuka kwa mwamuzi mwanamke mwenye mvuto ambaye pia ni mwanamitindo.
Mwamuzi huyo Elena Tambini, mwenye umri wa miaka 25 kwasasa ni mwamuzi wa ligi ndogo nchini humo lakini hiyo inaweza kuwa safari yake ya kuibukia katika Serie B na baadae Serie A na hata soka la kimataifa. Waamuzi wa kike wa kiwango cha juu ni adimu huku mwamuzi msaidizi Sian Massey ndiye mwamuzi pekee wa kike kuwepo katika orodha ya waamuzi wa kike katika Ligi Kuu nchini Uingereza.
No comments:
Post a Comment