GOLIKIPA wa klabu ya Olympiakos Roy Carroll amesema amstushwa na kuporomoka kwa klabu yake ya zamani Manchester United msimu huu. United walifanikiwa kupiga shuti moja pekee langoni wakati walipofungwa na Olympiakos katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa barani Ulaya hatua ya timu 16 bora uliochezwa wiki mbili zilizopita. Akihojiwa kabla ya kuelekea katika mchezo wao marudiano utakaofanyika Old Trafford leo usiku Carroll amesema hajawahi kuiona United ikishindwa kutengeneza nafasi hivyo lilikuwa jambo la kumstua kutoka na kiwango kibovu walichoonyesha. Carroll ambaye hakucheza katika mchezo huo wa kwanza, aliichezea United kwa miaka minne kuanzia mwaka 2001 mpaka 2005 akiisaidia timu hiyo kushinda taji la Ligi Kuu msimu 2002-2003 na Kombe la FA msimu uliofuata.
No comments:
Post a Comment