Friday, March 21, 2014

MKONGWE PIRLO AIBEBA JUVENTUS KUINGIA ROBO FAINALI YA EUROPA LEAGUE.

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu nchini Italia, Juventus jana walifanikiwa kusonga mbele katika hatua ya robo fainali ya michuano ya Europa League baada ya kufanikiwa kupata ushindi mwembamba dhidi ya Waitaliano wenzao Fiorentina. Bao pekee lililofungwa na kiungo mkongwe Andrea Pirlo lililotosha kuivusha Juventus katika hatua hiyo muhimu kwa jumla ya mabao 2-1 katika mechi mbili walizocheza. Kwa upande mwingine Waingereza pekee waliobakia katika michuano hiyo Tottenham Hotspurs walijikuta waking’olewa kwa jumla ya mabao 5-3 pamoja na kufanikiwa kutoka sare ya mabao 2-2 katika mchezo wa jana dhidi ya Benfica ya Ureno. Katika michezo mingine Waitaliano wengine katika michuano hiyo Napoli nao waliondoshwa katika michuano hiyo kwa jumla ya maba 3-2 baada ya kutoa sare ya mabao 2-2 na FC Porto ya Ureno huku Real Betis wakiwaondosha Wahispania wenzao Sevilla kwa changamoto ya mikwaju ya penati baada ya kutoka sare ya mabao 2-2 katika michezo miwili waliyokutana.

No comments:

Post a Comment