MENEJA wa klabu ya Valencia, Juan Antonio Pizzi amempongeza mshambuliaji wake kinda Paco Alcacer baada ya kufunga bao lingine dhidi ya Ludogorets na kuisaidia Valencia kupenya kirahisi katika robo fainali ya michuano ya Europa League. Kinga huyo ambaye amechukua nafasi ya nahodha wa zamani Roberto Soldado kufuatia kuhamia Tottenham Hotspurs, ameonekana kuyamudu vyema majukumu aliyopewa baada ya kufunga mabao katika mechi zote mbili walizokutana na mabingwa hao wa Bulgaria. Kufuatia kusonga mbele kwa timu hiyo Pizzi amedai kuwa nyota huyo mwenye umri wa miaka 20 yuko nyuma ya Lionel Messi na Cristiano Ronaldo wakati linapokuja suala la vipaji binafsi. Pizzi amesema ni ngumu kufanya anayofanya Alcacer na kama ukimfananisha na wachezaji wengine duniani kwa kiwango chake ni Messi na Ronaldo pekee ndio wako mbele yake.
No comments:
Post a Comment