MENEJA wa klabu ya Benfica ya Ureno amekiri kuwa Liverpool wameonyesha nia ya kutaka kumsajili mshambuliaji wao Rodrigo Moreno ambaye anakadiriwa kuwa na thamani ya paundi milioni 25. Wang’amua vipaji kutoka vilabu vya Manchester United, Chelsea na West Bromwich Albion walikuwa miongoni mwa wawakilishi kutoka Ligi Kuu ya Uingereza katika mchezo uliomalizika kwa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Tottenham Hotspurs huko Estadio da Luz jana usiku lakini Rodrigo mwenye umri wa miaka 23 hakucheza mechi hiyo. Akiulizwa kuhusu nia ya Liverpool kumtaka mshambuliaji huyo ambaye amefunga mabao 10 katika mechi 16 alizoichezea Benfica, Jesus amesema jambo hilo hilo ni kawaida kwasababu kila mchezaji wa timu hiyo anawindwa na vilabu vingine. Jesus amesema pamoja na Rodrigo kuwindwa na vilabu vingi lakini watajitahidi kujaribu kumbakisha klabuni hapo ili aweze kuendelea kuwasaidia kwasababu ameshakuwa sehemu muhimu katika kikosi chake.
No comments:
Post a Comment