MENEJA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amekataa nyongeza ya paundi milioni moja katika mshahara wake kwa mwaka kabla ya ya kutia saini ya kuongeza mkataba wake. Wenger anatarajiwa kusaini mkataba mpya wa miaka miwili kama ilivyofikiwa makubaliano na viongozi wa klabu hiyo Octoba mwaka jana. Kwa maana hiyo mkataba mpya wa kocha huyo utamuwezesha kulipwa kitita cha paundi milioni 7.5 kama ilivyokuwa katika mkataba wake unaomalizika baada ya Mfaransa huyo kukaa ofa ilitolewa na bodi ambayo ingemuwezesha kulipwa paundi milioni 8.5 kwa mwaka. Inaaminika kuwa Wenger ambaye ana mfuatia Jose Mourinho katika mameneja wanaolipwa pesa nyingi zaidi katika Ligi Kuu, anafikiri kuwa tayari ameshatunukiwa kwa kufanya kazi hiyo.
No comments:
Post a Comment