MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Inter Milan, Rodrigo Palacio amesema amefurahishwa baada ya kusaini mkataba mpya na vigogo hao wa Italia. Palacio mwenye umri wa miaka 32 alijiunga na Inter inayonolewa na kocha Walter Mazzarri katika kipindi cha majira ya kiangazi mwaka jana akitokea Genoa na amefunga mabao 12 katika mechi 27 alizoichezea klabu hiyo msimu huu. Kwa kiwango cha hali ya juu alichokionyesha katika kusifumania nyavu klabu hiyo imeamua kumzawadia mwaka mmoja zaidi ambao utamfanya kubakia hapo mpaka mwaka 2016. Nyota huyo wa kimataifa wa Argentina amesema kusaini mkataba huo mpya ni kama kutimiza ndoto zake hivyo anaahidi kufanya kila analoweza kuhakikisha anafanya vyema kuisaidia timu hiyo.

No comments:
Post a Comment