AFISA wa polisi wa zamani wa Afrika Kusini ameiambia mahakama inayosikiliza kesi ya mauaji ya mwanariadha mlemavu Oscar Pistorius kuwa saa mbili za mwanariadha huyo zilizpotea katika eneo la tukio. Ofisa huyo Schoombie van Renburg amesema alikasirishwa na kitendo hicho na kutoa amri kwa maofisa wake kukaguliwa kwa ajili ya kutafuta saa hizo. Mahakama pia ilionyesha picha ikimuonyesha Pistorius akiwa ametapakaa damu katika kaptura aliyokuwa amevaa siku ya tukio. Pistorius alikaa kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp kwa makusudi mwaka jana na kudai kuwa alifanya hivyo kwa kudhani kuwa ni jambazi limevamia kwake. Lakini waendesha mashitaka wamesema kuwa alimpiga risasi Steenkamp kwa makusudi baada ya kuzozana nyumbani kwake katika siku ya wapendanao mwaka jana.

No comments:
Post a Comment