LIGI Kuu ya Vodacom (VPL) inaendelea kesho (Machi 15 mwaka huu) kwa mechi tatu ambapo mabingwa watetezi Yanga wataumana na Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro. Nao vinara wa ligi hiyo, Azam wanaikaribisha Coastal Union ya Tanga katika mechi itakayofanyika Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi jijini Dar es Salaam. Mechi nyingine itachezwa Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba kwa kuwakutanisha wenyeji Kagera Sugar dhidi ya maafande wa Tanzania Prisons kutoka jijini Mbeya.

No comments:
Post a Comment