MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Real Madrid amefanikiwa kufikia rekodi ya mabao ya Ferenc Puskas aliyoweka katika klabu hiyo baada ya kufunga mabao mawili katika mchezo dhidi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Schalke usiku huu. Ronaldo ambaye ni mshindi wa tuzo mbili za Ballon d’Or alifunga bao la kwanza kwa timu yake katika dakika ya 21 na baadae kuongeza lingine baada ya Tim Hoogland kuisawazishia Schalke dakika ya 31 na kufikisha jumla ya mabao 242 katika mechi 236 alizocheza Madrid. Ronaldo mwenye umri wa miaka 29 alifikia rekodi hiyo akiwa amecheza Madrid kwa kipindi cha miaka mitatu pekee kulinganisha na miaka nane Puskas aliyoitumikia klabu hiyo. Mreno huyo kwasasa yuko katika nafasi ya nne ya katika orodha ya washambuliaji waliofunga mabao mengi zaidi wakiwa Madrid akiongozwa na Santillana mwenye mabao 290, Alfredo di Stefano mwenye mabao 307 na Raul mabao 323.
No comments:
Post a Comment