Tuesday, March 11, 2014

TIKETI 61,000 ZA FAINALI YA LIGI YA MABINGWA ULAYA KUUZWA.

ZAIDI theluthi moja kati ya tiketi 61,000 zitakazotolewa kwa ajili ya mchezo wa fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya utakaofanyika jijini Lisbon, Ureno Mei 24 mwaka huu wanatarajiwa kupewa maofisa, wadhamini na washirika wengine. Katika taarifa yake iliyotoka jana, Shirikisho la Soka barani Ulaya-UEFA limesema jumla ya tiketi 37,000 kati ya 61,000 zilizopo zitakwenda kwa mashabiki na jamii nzima kwa ujumla. UEFA iliemdelea kufafanua mgawanyo huo kuwa tiketi 24,000 zilizobakia zitapelekwa kwa waandaaji, UEFA wenyewe, Chama cha Soka cha Ureno, wadhamini wa matangazo na waandishi wa habari. Timu mbili zilizotinga fainali zenyewe zitapewa tiketi 17,000 kila moja kwa ajili ya mashabiki wao na tiketi 3,000 zitauzwa kwa mashabiki duniani kote kupitia mtandao wa UEFA.

No comments:

Post a Comment