Tuesday, March 11, 2014

MESSI WA BARCELONA TOFAUTI NA MESSI WA ARGENTINA.

NGULI wa soka wa Brazil, Pele amesema Lionel Messi huwa hachezi vizuri akiwa na timu yake ya taifa ya Argentina kama ilivyo anapokuwa Barcelona kutokana kushindwa kuelewana na wachezaji wenzake. Messi amekuwa akishambuliwa kwa kipindi kirefu na mashabiki wa soka nchini kwake ambao wanaamini kuwa nyota huyo huwa anajituma sana akiwa na Barcelona kuliko akivaa jezi ya timu yake ya taifa, lakini Pele ana mawazo tofauti kuhusu suala hilo. Pele mwenye umri wa miaka 73 amesema unapomuona Messi akicheza Barcelona anakuwa kweli ni mchezaji mzuri lakini akicheza katika timu ya taifa anakuwa Messi tofauti na aliyezieleka akiwa Hispania. Nguli aliendelea kusema kuwa kinachisababisha Messi kuwa ni kuzungukwa na wachezaji mahiri kama Xavi Hernandez na Andres Iniesta ambao humpa msaada mkubwa lakini akiwa na Argentina anakuwa tofauti kwasababu haelewani vyema na wachezaji wenzake.

No comments:

Post a Comment