Saturday, March 22, 2014

UFALME WA BARCELONA KUTAWALA SOKA LA HISPANIA UMEKWISHA - VALDANO.

MCHEZAJI na kocha wa zamani wa klabu ya Real Madrid Jorge Valdano anaamini kuwa ufalme wa Barcelona katika Ligi Kuu nchini Hispania maarufu kama La Liga unaelekea mwishoni wakati wenzao wakianza kuimarika. Barcelona wameshinda taji la La Liga mara nne katika misimu mitano iliyopita lakini kwasasa wako nyuma ya vinara Madrid kwa alama nne huku kukiwa kumebaki michezo 10 ukiwemo wa kesho. Valdano amesema Madrid ndio wenye nafasi kubwa kushinda mchezo huo wa kesho dhidi ya mahasimu wao Barcelona ambao wanaonekana kama wanaporomoka kiwango. Kocha huyo mwenye umr wa miaka 58 amesema mchezo huo unaipa nafasi Madrid kwa mara ya kwanza baada ya kupita kipindi kirefu. Mbali na kuipa nafasi Madrid, Valdano pia anakiri kikosi alichokuwa nacho kocha Gerardo Martino ni cha aina yake ingawa anadhani timu hiyo haiwezi kuvuna vipaji kama hivyo tena.

No comments:

Post a Comment