RAIS wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA, Sepp Blatter amesema michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2018 itachezwa kama ilivyopangwa nchini Urusi pamoja na mgogoro uliopo kuhusu jimbo la Crimea. Mapema mbunge wa Chama cha Labour, Andy Burnham aliiambia BBC kuwa FIFA inatakiwa kufikiria upya juu uamuzi wake wa kuipa Urusi uenyeji wa michuano hiyo. Lakini akiulizwa kuhusiana na suala hilo Blatter amesema kura zilipigwa kuipa uenyeji Urusi kuandaa michuano hiyo hivyo itafanyika kama ilivyopangwa. Rais wa Urusi Vladimir Putin alisaini mswada wa sheria jana kuhalalisha Urusi kulichukua jimbo hilo kutoka Ukraine. Hatua imekuja na kufuatiwa na vikwazo vipya vilivyowekwa na Umoja wa Ulaya na Marekani, lakini Blatter haoni kama hatua ya Urusi iliyochukua dhidi ya Crimea kama inaweza kuathiri michuano hiyo.
No comments:
Post a Comment